Elimu ni jumla ya maarifa aliyonayo mtu yanayomuwezesha kutatua changamoto za maisha yake ya kila siku. Elimu si ile tu inayopatikana shuleni na vyuoni bali ni maarifa yote yapatikanayo katika mazingira husika.
Elimu ni kitu muhimu sana ktk mapinduzi ya kifikra, kiuchumi na kimaendeleo. Elimu hubadili kabisa mfumo wa maisha ya jamii husika.
Elimu bora ni ile inayomfanya mtu ajitambue kwa kutambua thamani ya utu wake, kukabiliana na changamoto za maisha yake ya kila siku na kujiletea maendeleo.
Iwapo elimu inayotolewa haikidhi kutatua mahitaji na changamoto za maisha basi elimu hiyo haikidhi mahitaji ya jamii husika.
Hakuna elimu iliyo vuguvugu, bali elimu yaweza kutolewa kwa ajili ya ukombozi au kwa ajili ya uharibifu.
Mwandishi na mtaalam mmoja(mwafrika) wa mambo ya elimu, aliyeitwa “Paul Fraire” wa huko Amerika kusini alisema hivi:
“Education is never neutral, it must be for domestication or liberation”. Akimaanisha kuwa “hakuna elimu iliyo vuguvugu, bali yaweza kuwa kwa ajili ya udunishaji au Ukombozi”
Sasa tuulizane, elimu yetu inaangukia upande gani?
Kumbuka kuwa ili tukue kimaendeleo na kiuchumi, ni lazima tuwe na uwezo wa kuzalisha bidhaa zetu wenyewe kwa ajili ya soko la ndani na nje.
Ili tuzalishe bidhaa, ni lazima tuwe na wataalamu wa teknolojia yaani wagunduzi wa mashine na viwanda vidogo na hatimaye viwe viwanda vikubwa.
Tuwe na wanasayansi ili watutengenezee dawa, chemikali n.k.
Lazima tuwe na wakulima na wafugaji bora, n.k.
Ukienda shuleni leo, katika bara la Afrika ktk shule za msingi na sekondari na hata vyuoni ukawauliza wanafunzi wangependa kuwa watu gani hapo baadaye. Hakika utapata majibu haya: napenda kuwa nesi, mwalimu, mhasibu, derever, rubani, polisi, mwanajeshi, mwanasheria, waziri, rais, mbunge, n.k
Ni mara chache au utasikia wanafunzi wakisema wanataka kuwa mwanasayansi, mgunduzi, mtengeneza vifaa vya viwandani, fundi wa kuunda machine, mkulima, mfugaji au mgunduzi wa tiba bora kwa wanadamu! Ikumbukwe kuwa hili kundi la pili ndilo kundi lililoifanya Ulaya ikawa na mapinduzi ya viwanda!
Sikatai kuwa ajira zilizotajwa km uhasibu na upolisi n.k ni mbaya. Ninachosema ajira hizo ni kwa ajili ya watu walio tayari kutumia vitu au teknolojia iliyokwisha andaliwa. Lkn waandaaji lazima watoke kundi la pili.
Sasa, je, elimu yetu inatupeleka wapi?
Tujiulize, elimu inayotolewa barani Afrika inakidhi mahitaji ya mazingira yetu ya hapa Afrika au hapana? Kama tuna shule na vyuo vikuu, wagunduzi wetu wako wapi? Kwanini kila kifaa tunachotumia kinatoka ughaibuni?
Tuamke sasa, tubadili mifumo hii mibovu ya elimu tulitonayo. Afrika amka sasa!
Asanteni. Imeandaliwa na Pius Ntinya. Mwanamapinduzi wa Afrika .